USIKATE TAMAA YAKU BLOGGING KWA NAMNA YEYOTE

Kukata tamaa ya blogging ni rahisi sana
Mimi ninamaliza mwezi wa tisa mpaka wakati huu kwenye fani hii ya blogging, Njia ya kufikia hapa nilipo haikuwa raisi, japo kuwa siwezi sema kwamba mimi ni blogger mwenye mafanikio makubwa, napenda hatua niliyofikia kwa sababu naweza kuwapa watu maoni yangu ya vitu vingi tofauti.

Najua kwamba watu wengi sana wanaipenda hii fani ya blogging kwa sababu asili ya binadamu ni kupenda kuwa na sauti mbele za watu, na mtandao wakati huu ndio njia rahisi ya kufanya hivyo, japokuwa kuna sehemu kama facebookTwitter na JamiiForums, kuwa na sehemu ambayo unaweza ukaweka mawazo yako kwa sheria zako sio vibaya na hiyo ndiyo sababu kwanini nilitengeneza Riyadibhai.com. [ soma : Jinsi ya kufungua blog hatua kwa hatua ]

Kufungua blog siku hizi ni rahisi sana, unaweza ukafungua ya bure, lakini kwa wateja ambao nimewasaidia kuziweka website zao hewani na marafiki ninao wafahamu ndani ya jamii ya blogging, huwa wanaiacha hii fani baada ya miezi michache.

Sababu kwanini watu wanakata tamaa ya blogging

1. Kusikiliza maneno ya watu

Usiingie kwenye blogging huku ukitegemea kwamba kila mtu ataelewa mambo unayoandika, blogging kwa asilimia kubwa ni mtu anatumia maoni yake mwenye kuwaeleza watu wengi mtazamo wake, lazima watu wa kupinga watakuwa wengi.

Ila uzuri wake ni kwamba lazima na watu ambao watakaoelewa unachosema watakuwepo na kwa kawaida watukuwa ni wengi zaidi, andika unachotaka kuandika kwa sababu hamna mtu anayekukataza kutoa maoni yako.

Kuna mara nyingi maneno yanaweza kuwa ni ya watu waliokaribu, yaani ndugu na marafiki, wanaweza wakawa wanakwambia kwamba unapoteza muda wako na hayo ndio maneno ya watu wengi, Lakini wengi wao wanaongea tu kwa kufwata fikra zilizopitwa na wakati, hao ni watu wanaoiangalia Tanzania kwa mtazamo uliokwama.

2. Kujiandaa kipesa kulipia mahitaji ya blogging
Kama unatumia huduma za bure kama blogger, unaweza usielewe kuhusu maswala ya hosting na Domains, Kama unataka uzame kweli kwenye fani ya blogging, lazima kuna muda inabidi ufanye maamuzi ya kulipia ili kupata uwezo zaidi wa kufanya chochote unachotaka kwenye blog yako.

Kama haujajipanga vizuri kwa malipo ambayo itabidi uwe unafanya kila baada ya muda flani, unaweza ukakata tamaa, Tatizo ni kwamba watu huwa wanaingia “mguu mmoja nje” ndio maana kufanya bajeti kwa ajili ya blogging kwao ni ngumu.

Kama kweli unampango na blogging, iwe hobby tu au unataka uingie kwa nia ya kibiashara zaidi, hakikisha pia unafikiria swala la malipo ambayo inabidi uyafanye.

3. Kuingia bila ushauri wa nini cha kufanya kwanza
Ni vitu vichache sana vizuri hapa duniani utakavyo vipata kwa kuparamia, blogging sio moja ya vitu hivyo, kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kabla haujaingia hata kufungua website.

Kuanzia hatua ya kuchagua jina tu la website yako mbaka hatua ngumu kama za kuboresha mwonekano wa website yako, ni lazima utulie na kama ni mgeni kabisa wa mambo kama hayo, lazima umtafute mtu anayeelewa vizuri kuhusu mambo hayo.

Sio lazima uende kwa watu wanaotoza hela, hata kufanya tu uchunguzi kwenye kwenye sehemu kama Youtube inaweza ikakuokoa mambo mengi sana mabaya kwenye safari yako.

[ soma : Mambo muhimu ya kufahamu kabla na baada ya kufungua blog ]

4. Kuiga mno website zilizofanikiwa
Hili swala lipo na watu wengi sana wanaongia kwenye fani ya blogging bila kufikiria kwanza ni nini wanataka kuwasilisha kwa wasomaji wao,  watu wengi wakishakwama kwenye nini waandike, huwa hawafikirii kuanza kutafuta msaada au ushauri popote, huwa wanakimbilia kuiga website zilizofanikiwa kama zotekali.com au nyingine za aina hiyo.

Blog za aina hii hazijaweza kufanikiwa kwa sababu nyingi sana, ambazo ziko wazi ni kama blog hiyo itakuwa haina wasomaji kwa sababu watakachokuta ndani stori zilizojirudia tu.

Kuendesha blog kwa kutegemea blog ya mtu mwingine ni sawa sawa na mtu anayetaka kuhamia kwenye nyumba bila ya kuwa na mali zozote huku akitegemea kila kitu kutoka kwa jirani, kwa staili kama hiyo hautaweza fika popote na blogging.

5. Kuingia na mategemeo makubwa mno
Usiingie kwenye fani ya blogging huku unajenga mategemeo ya kwamba siku ya kwanza utakayoweka post yako, watu laki tano wataingia kusoma, Kipindi unaingia kwenye blogging akili yako yoyote inabidi iwe kwenye kuhakikisha mambo unayoweka ndani ya blog yako, ni ambayo hata wewe unaweza ukafurahi ukiyasoma.

Kama unawatu hata wawili, hata kama ni ndugu zako tu unawapa kila siku wasome post zako, hakikisha basi kila unapoingia kuandika post yako mpya, unalenga kuwafurahisha hao watu, Lazima baada ya muda watu wataendelea kuja kama utahakikisha tu unaandika mambo watu wanayotaka kuyasoma.

Mwisho
Safari ya blogging sio rashisi, lakini maneno hayo tunaweza tukayasema kwenye kitu chochote hapa duniani na yakawa kweli, Kama kweli unaona ni kitu unachopenda kufanya basi hakikisha vikwazo vidogo kama nilivyoviweka hapo juu sio vitakavyokuangusha.

Umeweza kupata kitu kizuri kupitia post hii unaweza ukaniachia maoni yako kwenye sehemu ya comments hapo chini.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa